Jarida la Mapishi

Keki ya ndizi na chocolate

Keki ya ndizi na chocolate | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 30
  • Kupika
    Dakika 45
  • Walaji
    12

Keki ya ndizi na chocolate, ni keki yenye mchanganyiko wa ladha tamu ya ndizi mbivu pamoja na chocolate. Keki hii yaweza kuliwa kama kitindamlo, au kama kitafunio pamoja na chai au kahawa. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika keki hii ya ndizi na chocolate.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, unga wa ngano, baking soda, pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri.

    Step2

    Chukua bakuli nyingine ndogo. Weka ndani ya hiyo bakuli siagi, sukari, na uchanganye vizuri, kisha weka mayai, vanilla extract, pamoja na ndizi mbivu, halafu endelea kuchanganya.

    Step3

    Chukua mchanganyiko wa bakuli ndogo ya pili, na umimine kwenye mchanganyiko wa bakuli la kwanza. Weka jozi (walnuts), pamoja na dark chocolate chips kwenye hilo bakuli la kwanza, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

    Step4

    Chukua sufuria la kuoka keki (cake pan) lenye ukubwa wa nchi 9, na upake siagi. Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka keki.

    Step5

    Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka keki ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 40 mpaka 45, au hadi utakapo ona keki imeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step6

    Keki ikisha iva, iondoe kwenye jiko la kuoka, kisha iweke pembeni ili ipoe, ikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka keki. Keki ikishapoa, unaweza kuitoa ndani ya sufuria la kuoka keki, na kuikata kwa ajili ya kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.