Jarida la Mapishi

Ice cream ya kahawa

Ice cream ya kahawa | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 35
  • Kupika
    -
  • Walaji
    2

Ice cream ya kahawa, ni ice cream inayo tengenezwa kwa kutumia, kahawa ya unga, maziwa, pamoja na krimu. Ice cream hii yafaa kula kama kitindamlo, baada ya chakula cha jioni. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza ice cream hii ya kahawa.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria ndogo. Weka ndani ya hiyo sufuria kahawa pamoja na maji, kisha changanya vizuri. Weka maziwa pamoja double cream, halafu chemsha kwenye jiko lenye moto mdogo huku ukikoroga hadi utakapo ona imeanza kuchemka, kisha epua na uweke pembeni.

    Step2

    Chukua bakuli ndogo. Weka ndani ya hilo bakuli mayai pamoja na sukari, kisha changanya kwa kupiga piga mchanganyiko huo, hadi utakapo ona umechanganyika vizuri na kuwa laini. Mimina mchanganyiko huu kwenye sufuria lenye mchanganyiko wa kahawa, kisha koroga vizuri.

    Step3

    Chukua sufuria kubwa lenye maji ya moto. Weka sufuria lenye mchanganyiko wa kahawa ndani ya sufuria lenye maji ya moto, kisha piga piga mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 10.

    Step4

    Ondoa sufuria hilo lenye mchanganyiko wa kahawa kutoka kwenye sufuria lenye maji ya moto, kisha mimina mchanganyiko huo kwenye kontena. Funika vizuri kontena hilo halafu liweke kwenye friji kwa muda wa saa 4.

    Step5

    Baada ya saa 4, ondoa kontena hilo kwenye friji, kisha mimina mchanganyiko huo wa ice cream kwenye mashine ya kutengenezea ice cream (Ice Cream Maker Cooler). Washa mashine hiyo kwa muda wa dakika 40, au hadi utakapo ona ice cream imekuwa nzito na laini.

    Step6

    Ondoa ice cream hiyo kutoka kwenye mashine ya kutengeneza ice cream, kisha pakua kwenye bakuli safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.