Jarida la Mapishi

Ice cream ya minti na chocolate

 • Maandalizi
  Dakika 25
 • Kupika
  -
 • Walaji
  2

Ice cream ya minti na chocolate, ni ice cream ambayo hutengenezwa kwa kutumia majani ya minti aina ya peppermint pamoja na dark chocolate chips. Ice cream hii yafaa kula kama kitindamlo baada ya chakula cha jioni. Fuata hatua fuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza ice cream hii ya minti na chocolate.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria kubwa. Weka ndani ya hilo sufuria maziwa, majani ya minti, pamoja na dark chocolate chips kisha chemsha mchanganyiko huo kwenye jiko lenye moto wa wastani huku ukikoroga mara kwa mara. Ukiona maziwa yameanza kuchemka, epua na uweke pembeni ili yapoe.

  Step2

  Chukua chujio na uchuje maziwa ili kuondoa majani ya minti yaliyomo kwenye maziwa na kubakiwa na maziwa peke yake.

  Step3

  Chukua bakuli ndogo. Weka ndani ya hilo bakuli viini vya mayai pamoja na sukari, kisha piga piga, mchanganyiko huo hadi utakapo ona umechanganyika vizuri na kuwa laini. Mimina mmchanyiko huu kwenye bakuli lenye maziwa halafu koroga vizuri.

  Step4

  Chukua sufuria kubwa. Weka maji ya moto kwenye hilo sufuria. Weka mchanganyiko wa maziwa ulio uchemsha ndani ya hilo sufuria lenye maji ya moto, kisha changanya kwa kupiga piga mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 10.

  Step5

  Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena mchanganyiko wa maziwa ulio upiga piga, kisha funika vizuri kontena hilo na uliweke kwenye friji kwa muda wa saa 3.

  Step6

  Baada ya saa 3, ondoa kontena hilo kwenye friji, kisha mimina mchanganyiko huo wa ice cream kwenye mashine ya kutengenezea ice cream (Ice Cream Maker Cooler). Washa mashine hiyo kwa muda wa dakika 40, au hadi utakapo ona ice cream imekuwa nzito na laini.

  Step7

  Ondoa ice cream hiyo kutoka kwenye mashine ya kutengeneza ice cream, kisha pakua kwenye bakuli safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *