Jarida la Mapishi

Ice cream ya mchaichai na nazi

Ice cream ya mchaichai na nazi | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 20
  • Kupika
    -
  • Walaji
    3

Ice cream ya mchaichai na nazi, ni ice cream ambayo asili yake ni kutoka nchini Italia. Ice cream hii hutengenezwa kwa kutumia majani halisi ya mchaichai pamoja na tui la nazi. Ice cream hii yafaa kula kama kitindamlo baada ya mlo wowote ule. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza ice cream hii ya mchaichai na nazi.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria ndogo. Weka kwenye hilo sufuria, tui la nazi, double cream, pamoja na majani ya mchaichai, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10.

    Step2

    Weka sukari pamoja na powderered sugar, kisha endelea kukoroga hadi utakapo ona sukari yote imeyeyuka. Epua mchanganyiko huo na uweke pembeni ili upoe.

    Step3

    Chukua limao 1 na ukune (grate) maganda yake yote, kisha weka maganda hayo kwenye sufuria lenye mchanganyiko wa tui la nazi.

    Step4

    Chukua limao ulilokuna maganda yake pamoja na malimao mengine yaliyobakia. Kamua vizuri malimao hayo na umimine juisi yake kwenye sufuria lenye mchanganyiko wa tui la nazi, kisha koroga vizuri.

    Step5

    Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena mchanganyiko uliomo kwenye sufuria, kisha funika vizuri kontena hilo na uliweke kwenye friji kwa muda wa saa 1.

    Step6

    Baada ya saa 1, ondoa kontena hilo kwenye friji, kisha chuja mchanganyiko huo kwa kutumia chujio. Mimina mchanganyiko huo wa ice cream kwenye mashine ya kutengenezea ice cream (Ice Cream Maker Cooler), kisha washa mashine hiyo kwa muda wa dakika 40, au hadi utakapo ona ice cream imekuwa nzito na laini.

    Step7

    Ondoa ice cream hiyo kutoka kwenye mashine ya kutengeneza ice cream, kisha pakua kwenye bakuli safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.