Jarida la Mapishi

Ice cream ya nazi na mtindi

 • Maandalizi
  Dakika 15
 • Kupika
  -
 • Walaji
  2

Ice cream ya nazi na mtindi, ni ice cream rahisi sana kutengeneza, ambayo hutengenezwa kwa kutumia tui la nazi, mtindi, pamoja na krimu. Ice cream hii yafaa kula kama kitindamlo kwenye msimu wa kiangazi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza ice cream hii ya nazi na mtindi.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua kikaango kikubwa. Weka nazi iliyo kunwa kwenye hicho kikaango, kisha kaanga hadi utakapo nazi hiyo imebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step2

  Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena, mtindi, tui la nazi , double cream, sukari, pamoja na nazi uliyo ikaanga, halafu changanya vizuri, kisha funika vizuri kontena hilo na uliweke kwenye friji kwa muda wa dakika 5 mpaka 10.

  Step3

  Baada ya dakika 5 au 10, ondoa kontena hilo kwenye friji, kisha mimina mchanganyiko huo wa ice cream kwenye mashine ya kutengenezea ice cream (Ice Cream Maker Cooler). Washa mashine hiyo kwa muda wa dakika 45, au hadi utakapo ona ice cream imekuwa nzito na laini.

  Step4

  Ondoa ice cream hiyo kutoka kwenye mashine ya kutengeneza ice cream, kisha pakua kwenye bakuli safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *