Jarida la Mapishi

Keki ya blueberry

Keki ya blueberry | Jarida la Mapishi
 • Maandalizi
  Dakika 15
 • Kupika
  Dakika 45
 • Walaji
  12

Keki ya blueberry, ni keki tamu ambayo hupikwa kwa kutumia matunda ya blueberry yalioiva. Keki hii yafaa kuliwa katika hafla yoyote ile hasa Birthday. Fuata jatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika keki hii ya blueberry.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, siagi, sukari, pamoja na light brown sugar, kisha changanya vizuri.

  Step2

  Weka mayai, limao iliyo kamuliwa, buttermilk na maganda ya limao yaliyo kunwa, halafu endelea kuchanganya.

  Step3

  Weka unga wa ngano, baking powder, chumvi, pamoja na matunda ya blueberry, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

  Step4

  Chukua sufuria la kuoka keki (cake pan) lenye ukubwa wa nchi 10, na upake siagi. Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka keki.

  Step5

  Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka keki ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 40 mpaka 45, au hadi utakapo ona keki imeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step6

  Keki ikisha iva, iondoe kwenye jiko la kuoka, kisha iweke pembeni ili ipoe, ikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka keki. Keki ikishapoa, unaweza kuitoa ndani ya sufuria la kuoka keki, na kuikata kwa ajili ya kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *


  The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.