Jarida la Mapishi

Ice cream ya ndizi

Ice cream ya ndizi | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 40
  • Kupika
    -
  • Walaji
    2

Ice cream ya ndizi, ni ice cream tamu na yenye krimu, inayo tengenezwa kwa kutumia ndizi mbivu. Ice cream hii yafaa sana kula baada ya kifungua kinywa wakati wa asubuhi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza ice cream hii ya ndizi.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria ndogo. Weka maziwa kwenye kwenye hilo sufuria, kisha weka sufuria hilo kwenye jiko na uache maziwa yachemke. Ukiona maziwa yamechemka, epua na uyaweke pembeni.

    Step2

    Chukua bakuli. Weka ndani ya hiyo bakuli, viini vya mayai pamoja sukari, kisha piga piga mchanganyiko huo vizuri kwa kutumia kijiko. Mimina maziwa kwenye mchanganyiko huo na ukoroge vizuri.

    Step3

    Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria maji ya moto. Weka bakuli lenye mchanganyiko wa sukari, mayai na maziwa ndani ya hilo sufuria lenye maji ya moto, kisha endelea kuchanganya mchanganyiko huo uliomo kwenye bakuli kwa kupiga piga kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona mchanganyiko huo umekuwa laini.

    Step4

    Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena mchanganyiko uliochanganya kwenye bakuli, kisha funika vizuri kontena hilo na uliweke kwenye friji kwa muda wa saa 4.

    Step5

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka ndizi kwenye hiyo mashine ya kusaga, kisha saga hadi utakapo ona ndizi hizo zimesagika vyema na kuwa laini.

    Step6

    Chukua bakuli ndogo. Weka ndani ya hilo bakuli ndizi ulizo zisaga pamoja na double cream, kisha changanya vizuri, halafu weka pembeni. Baada ya saa 4, mimina mchanganyiko huu kwenye kontena uliloliweka kwenye friji, kisha changanya vizuri.

    Step7

    Mimina mchanganyiko huo wa ice cream kwenye mashine ya kutengenezea ice cream (Ice Cream Maker Cooler). Washa mashine hiyo kwa muda wa dakika 40, au hadi utakapo ona ice cream imekuwa nzito na laini.

    Step8

    Ondoa ice cream hiyo kutoka kwenye mashine ya kutengeneza ice cream, kisha pakua kwenye bakuli safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Recipe Reviews

    • Joyce Wadelanga

      Asante kwa somo zuri

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.