Jarida la Mapishi

Muffins za jozi na ndizi

Muffins za jozi na ndizi | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 40
  • Kupika
    Dakika 20
  • Walaji
    12

Muffins za jozi na ndizi, ni muffins tamu ambazo hupikwa kwa kutumia njugu za jozi zilizo katwa katwa pamoja na ndizi mbivu zilizo katwa katwa pia. Muffins hizi zafaa sana kula kama kifungua kinywa wakati wa asubuhi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika muffins hizi za jozi na ndizi.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, ndizi, light brown sugar, mayai, mtindi, pamoja na siagi, kisha changanya vizuri.

    Step2

    Weka unga wa ngano, jozi zilizo sagwa, chumvi, baking powder, pamoja na jozi zilizo katwa katwa, kisha changanya vizuri kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

    Step3

    Chukua sufuria la kuoka muffins (muffins pan), lenye matundu 12 ya muffins, na uweke ndani ya hayo matundu karatasi za kuokea muffin (muffin papers). Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka muffins.

    Step4

    Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka muffins ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona muffins zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step5

    Muffins zikisha iva, ziondoe kwenye jiko la kuoka, kisha ziweke pembeni ili zipoe, zikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka muffins. Muffins zikishapoa, unaweza kuzitoa ndani ya sufuria la kuoka muffins, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.