Jarida la Mapishi

Ice cream ya pistachio

Ice cream ya pistachio | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 40
  • Kupika
    -
  • Walaji
    2

Ice cream ya pistachio, ni ice cream tamu yenye rangi ya kijani ambayo hutengenezwa kwa kutumia njugu mbichi za pistachio zilizo menywa maganda na kusagwa. Ice cream hii yafaa kula kama kitindamlo baada ya mlo wowote ule. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza ice cream hii ya pistachio.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka pistachios kwenye hiyo mashine ya kusaga, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri.

    Step2

    Chukua sufuria ndogo. Weka kwemye hiyo sufuria, maziwa, double cream, pamoja na pistachio ulizo zisaga, kisha chemsha mchanganyiko huo kwenye jiko lenye moto mkubwa huku ukikoroga. Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, halafu acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 5 zaidi, kisha epua na uweke pembeni.

    Step3

    Chukua bakuli ndogo. Weka ndani ya hilo bakuli, viini vya mayai pamoja na sukari, kisha changanya vizuri. Mimina mchanganyiko huu kwenye sufuria lenye mchanganyiko wa maziwa, halafu koroga vizuri.

    Step4

    Chukua sufuria kubwa. Weka maji ya moto kwenye hilo sufuria. Weka mchanganyiko wa maziwa ulio uchemsha ndani ya hilo sufuria lenye maji ya moto, kisha changanya kwa kupiga piga mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 10.

    Step5

    Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli maji ya baridi pamoja na vipande vya barafu (ice cubes). Ondoa sufuria ndogo ulilo liweka ndani ya sufuria kubwa lenye maji ya moto, halafu weka sufuria hilo ndani ya hili bakuli lenye maji ya baridi, kisha koroga mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 10.

    Step6

    Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena mchanganyiko wa maziwa ulio upiga piga, kisha funika vizuri kontena hilo na uliweke kwenye friji kwa muda wa saa 1.

    Step7

    Baada ya saa 1, ondoa kontena hilo kwenye friji. Weka limao ndani ya mchanganyiko huo, halafu koroga vizuri.

    Step8

    Mimina mchanganyiko huo wa ice cream kwenye mashine ya kutengenezea ice cream (Ice Cream Maker Cooler). Washa mashine hiyo kwa muda wa dakika 40, au hadi utakapo ona ice cream imekuwa nzito na laini.

    Step9

    Ondoa ice cream hiyo kutoka kwenye mashine ya kutengeneza ice cream, kisha pakua kwenye bakuli safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.