Jarida la Mapishi

Cupcakes za nazi

 • Maandalizi
  Saa 1 Dk. 10
 • Kupika
  Dakika 20
 • Walaji
  12

Cupcakes za nazi, ni cupcakes tamu zilizo sheheni ladha ya nazi. Cupcakes hizi hupikwa kwa kutumia tui la nazi pamoja na nazi iliyokunwa. Cupcakes hizi yafaa kula kwenye birthday au kwenye sherehe nyingine yoyote ile. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika cupcakes hizi za nazi.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, siagi, sukari, pamoja na vanilla extract, kisha changanya vizuri.

  Step2

  Weka mayai, halafu endelea kuchanganya.

  Step3

  Weka unga wa ngano, baking powder, chumvi, nazi iliyo kunwa, pamoja na tui la nazi, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

  Step4

  Chukua sufuria la kuoka cupcakes (cupcakes pan) lenye matundu 12 ya cupcakes, na uweke ndani ya hayo matundu karatasi za kuokea cupcake (cupcake papers). Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka cupcakes.

  Step5

  Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka cupcakes ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 15 mpaka 20, au hadi utakapo ona cupcakes zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step6

  Cupcakes zikisha iva, ziondoe kwenye jiko la kuoka, kisha ziweke pembeni ili zipoe, zikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka cupcakes. Cupcakes zikishapoa, unaweza kuzitoa ndani ya sufuria la kuoka cupcakes, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *