Jarida la Mapishi

Keki ya jozi na viungo

 • Maandalizi
  Dakika 20
 • Kupika
  Dakika 40
 • Walaji
  8

Keki ya jozi na viungo, ni keki tamu ambayo hupikwa kwa kutumia jozi zilizo katwa katwa pamoja na viungo mbali mbali, kama vile mdalasini na tangawizi. Keki hii yafaa sana kula kama kitindamlo kwenye msimu wa vuli. Fuata hatua zifuatazo, ili ujiifunze jinsi ya kupika keki hii ya jozi na viungo.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, mayai pamoja na sukari, kisha changanya vizuri.

  Step2

  Weka mafuta ya kupikia, halafu endelea kuchanganya.

  Step3

  Weka jozi, mdalasini, tangawizi, iliki, unga wa ngano, chumvi, pamoja na baking soda, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

  Step4

  Chukua sufuria la kuoka keki (cake pan) lenye ukubwa wa nchi 8, na upake siagi. Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka keki.

  Step5

  Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka keki ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 35 mpaka 40, au hadi utakapo ona keki imeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step6

  Keki ikisha iva, iondoe kwenye jiko la kuoka, kisha iweke pembeni ili ipoe, ikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka keki. Keki ikishapoa, unaweza kuitoa ndani ya sufuria la kuoka keki, na kuikata kwa ajili ya kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *