-
MaandaliziSaa 1 Dk. 10
-
KupikaDakika 20
-
Walaji16
Cupcakes za viungo, ni cupcakes tamu na rahisi kupika zilizo sheheni ladha ya viungo, ambazo hupikwa kwa kutumia viungo vya aina mbali mbali, kama vile, mdalasini na iliki. Cupcakes hizi zafaa sana kuliwa katika sherehe za msimu wa vuli. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika cupcakes hizi za viungo.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, siagi, pamoja na sukari, kisha changanya vizuri.
Weka mayai, mtindi na vanilla extract, halafu endelea kuchanganya.
Weka unga wa ngano, mdalasini, tangawizi, iliki, chumvi, pamoja na baking powder, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sufuria la kuoka cupcakes (cupcakes pan) lenye matundu 12 ya cupcakes, na uweke ndani ya hayo matundu karatasi za kuokea cupcake (cupcake papers). Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka cupcakes.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka cupcakes ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona cupcakes zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Cupcakes zikisha iva, ziondoe kwenye jiko la kuoka, kisha ziweke pembeni ili zipoe, zikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka cupcakes. Cupcakes zikishapoa, unaweza kuzitoa ndani ya sufuria la kuoka cupcakes, tayari kwa kula.
Leave a Review