Jarida la Mapishi

Chai ya iliki

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 5
 • Walaji
  2

Chai ya iliki, ni kinywaji maarufu sana hasa katika nchi za India na Tanzania. Chai hii hupikwa kwa kutumia majani ya chai, maziwa, pamoja na iliki. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika chai hii ya iliki.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria la ukubwa wa wastani. Weka kwenye hilo sufuria, maji, maziwa, pamoja na iliki ya unga, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.

  Step2

  Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo. Weka majani ya chai halafu koroga vizuri, kisha acha iendelee kuchemka kwa muda wa sekunde 30 mpaka dakika 1, kisha epua na uweke pembeni.

  Step3

  Chukua vikombe 2 pamoja na chujio. Chuja chai ndani ya hivyo vikombe. Weka sukari kadiri ya mahitaji yako, kisha koroga vizuri, tayari kwa kunywa.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *