-
Maandalizi-
-
Kupika-
-
Walaji2
Lemonade, ni kinywaji kitamu, chenye ladha ya uchachu na cha kuburudisha ambacho hutengenezwa hasa kwa kutumia malimao, maji, pamoja na sukari. Kinywaji hiki cha lemonade chafaa sana kunywa katika kipindi cha joto. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza lemonade hii.
Ingredients
Directions
Step1
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, malimao, matunda ya apple, maji, pamoja na sukari, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.
Step2
Chukua chujio, kisha chuja lemonade hiyo vizuri.
Step3
Mimina lemonade kwenye chombo safi, kisha iweke kwenye friji ili ipate baridi, kabla ya kunywa.
Conclusion
Unaweza kuongeza maji zaidi, endapo utaona maji yaliyomo katika lemonade hii ni kidogo.
Leave a Review