Jarida la Mapishi

Keki ya ndizi

 • Maandalizi
  Dakika 20
 • Kupika
  Dakika 35
 • Walaji
  8

Keki ya ndizi, ni moja wapo ya keki ambazo ni rahisi sana kupika. Keki hii hupikwa kwa kutumia ndizi mbivu, unga wa ngano, maziwa pamoja na siagi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika keki hii ya ndizi.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, unga wa ngano, baking soda, pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri.

  Step2

  Chukua bakuli nyingine ndogo. Weka ndani ya hiyo bakuli, siagi, sukari, dark brown sugar, pamoja na mayai, na uchanganye vizuri, kisha weka ndizi mbivu, halafu endelea kuchanganya.

  Step3

  Chukua mchanganyiko wa bakuli ndogo ya pili, na umimine kwenye mchanganyiko wa bakuli la kwanza, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kuchanganyia, kisha weka dark chocolate chips ndani ya huo mchanganyiko na ukoroge vizuri.

  Step4

  Chukua sufuria la kuoka keki (cake pan) lenye ukubwa wa nchi 9, na upake siagi. Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka keki.

  Step5

  Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka keki ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 30 mpaka 35, au hadi utakapo ona keki imeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step6

  Keki ikisha iva, iondoe kwenye jiko la kuoka, kisha iweke pembeni ili ipoe, ikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka keki. Keki ikishapoa, unaweza kuitoa ndani ya sufuria la kuoka keki, na kuikata kwa ajili ya kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *