Jarida la Mapishi

Ice cream ya kiwi

 • Maandalizi
  Dakika 15
 • Kupika
  -
 • Walaji
  4

Ice cream ya kiwi, ni ice cream rahisi kutengeneza, ambayo hutengenzezwa kwa kutumia tunda halisi la kiwi lililo sagwa. Ice cream hii yafaa sana kula kwenye sherehe ya aina yotote ile. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza ice cream hii ya kiwi.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, matunda ya kiwi, applesauce, sukari, pamoja na juisi ya apple, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

  Step2

  Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hiyo bakuli, ute wa mayai pamoja na limao iliyo kamuliwa, kisha changanya vizuri mchanganyiko huo kwa kuupiga piga. Mimina mchanganyiko ulio usaga, kisha changanya vizuri.

  Step3

  Mimina mchanganyiko huo wa ice cream kwenye mashine ya kutengenezea ice cream (Ice Cream Maker Cooler). Washa mashine hiyo kwa muda wa dakika 45 mpaka 60, au hadi utakapo ona ice cream imekuwa nzito na laini.

  Step4

  Ondoa ice cream hiyo kutoka kwenye mashine ya kutengeneza ice cream, kisha pakua kwenye bakuli safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *