Jarida la Mapishi

Juisi ya apple

 • Maandalizi
  Dakika 10
 • Kupika
  -
 • Walaji
  1

Juisi ya apple, ni juisi tamu iliyosheheni virutubisho vingi muhimu, vinavyoweza kukusaidia kukuweka sawa na kuwa na afya njema mwaka mzima. Juisi hii ni rahisi sana kutengeneza na unaweza kuitengeneza nyumbani kwako kwa muda mfupi tu, ndani ya dakika 10. Fuata hatua zifuatazo, ili kujifunza jinsi ya kutengeneza juisi hii ya apple.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Osha vizuri matunda ya apple kwenye maji yanayo tiririka, kisha uyamenye maganda yake. Kata kila tunda la apple katika vipande 4 na uondoe mbegu zilizomo ndani ya matunda hayo ya apple.

  Step2

  Weka vipande hivyo vya apple kwenye mashine ya kusaga (blender), pamoja na sukari, maji na limao iliyo kamuliwa, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wa juisi umesagika vyema.

  Step3

  Chuja juisi kwa kutumia chujio, kisha iweke kwenye friji ili ipate baridi kabla ya kunywa.

  Conclusion

  Unaweza kuongeza maji kwenye juisi hii kadiri upendavyo, endapo utaona maji yaliyomo katika juisi hii kidogo.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *