Jarida la Mapishi

Ice cream ya strawberry

Ice cream ya strawberry | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 25
  • Kupika
    -
  • Walaji
    2

Ice cream ya strawberry, ni ice cream tamu inayo tengenezwa kwa kutumia strawberry, krimu na sukari. Ice cream hii hutengenezwa kwa kutumia matunda halisi ya strawberry, tofauti na ice cream nyingine za strawberry ambazo huwekewa ladha ya strawberry. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza ice cream hii ya strawberry.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, matunda ya strawberry, double cream, jam ya strawberry, sukari, maji, pamoja na limao, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vyema na kuwa laini.

    Step2

    Mimina mchanganyiko huo wa ice cream ulio usaga kwenye mashine ya kutengenezea ice cream (Ice Cream Maker Cooler). Washa mashine hiyo kwa muda wa dakika 50, au hadi utakapo ona ice cream imekuwa nzito na laini.

    Step3

    Ondoa ice cream hiyo kutoka kwenye mashine ya kutengeneza ice cream, kisha pakua kwenye bakuli safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.