Jarida la Mapishi

Ice cream ya biskuti

 • Maandalizi
  Dakika 45
 • Kupika
  -
 • Walaji
  2

Ice cream ya biskuti, ni ice cream yenye ladha nzuri ya biskuti ambayo hutengenezwa kwa kutumia biskuti zilizo sagwa pamoja na krimu. Ice cream hii yafaa zaidi kula kama kitindamlo baada ya mlo wowote ule. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza ice cream hii ya biskuti.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli ndogo. Weka ndani ya hiyo bakuli bisukuti zilizo sagwa pamoja na almond milk, halafu changanya vizuri kisha weka pembeni kwa muda wa dakika 30.

  Step2

  Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli mtindi, sukari, vanilla sugar, pamoja na double cream, kisha changanya vizuri kwa kuupiga piga mchanganyiko huo.

  Step3

  Mimina mchanganyiko wa bakuli ndogo ya kwanza kwenye mchanganyiko wa kontena kubwa, kisha changanya vizuri. Funika vizuri kontena hilo na uliweke kwenye friji kwa muda wa saa 4.

  Step4

  Baada ya saa 4, ondoa kontena hilo kwenye friji, kisha mimina mchanganyiko huo wa ice cream kwenye mashine ya kutengenezea ice cream (Ice Cream Maker Cooler). Washa mashine hiyo kwa muda wa dakika 40, au hadi utakapo ona ice cream imekuwa nzito na laini.

  Step5

  Ondoa ice cream hiyo kutoka kwenye mashine ya kutengeneza ice cream, kisha pakua kwenye bakuli safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *