Jarida la Mapishi

Ice cream ya pilipili na chocolate

 • Maandalizi
  Dakika 15
 • Kupika
  -
 • Walaji
  4

Ice cream ya pilipili na chocolate, ni ice cream yenye ladha tamu ya chocolate na muwasho wa pilipili kwa mbali. Ice cream hii yafaa kula kama kitindamlo, baada ya chakula cha jioni. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza ice cream ya pilipili na chocolate.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria ndogo. Weka ndani ya hilo sufuria maziwa pamoja na cocoa powder, kisha chemsha mchanganyiko huo wa maziwa kwenye jiko lenye moto wa wastani. Ukiona imeanza kuchemka, epua na uweke pembeni ili ipoe.

  Step2

  Chukua bakuli kubwa. Weka double cream ndani ya hilo bakuli, kisha changanya double cream hiyo kwa kuipiga piga, hadi utakapo ona imekuwa nzito. Mimina mchanganyiko huu kwenye sufuria lenye mchanganyiko wa maziwa.

  Step3

  Weka asali pamoja na pilipili ya unga, kisha koroga vizuri.

  Step4

  Mimina mchanganyiko huo wa ice cream kwenye mashine ya kutengenezea ice cream (Ice Cream Maker Cooler). Washa mashine hiyo kwa muda wa dakika 40, au hadi utakapo ona ice cream imekuwa nzito na laini.

  Step5

  Ondoa ice cream hiyo kutoka kwenye mashine ya kutengeneza ice cream, kisha pakua kwenye bakuli safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *