Jarida la Mapishi

Keki ya viazi vitamu

 • Maandalizi
  Dakika 50
 • Kupika
  Dakika 40
 • Walaji
  10

Keki ya viazi vitamu, ni keki inayopikwa kwa kutumia viazi vitamu vilivyo sagwa na mdalasini. Keki hii yafaa sana kula katika kipindi cha sikukuu. Keki hii yaweza pia kuliwa wakati wowote. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika keki hii ya viazi vitamu.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, viazi vitamu, maganda ya chungwa, mafuta ya kupikia, mayai, light brown sugar, pamoja na vanilla extract, kisha changanya vizuri.

  Step2

  Weka mdalasini, chumvi, unga wa ngano, baking powder, pamoja na baking soda, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

  Step3

  Chukua sufuria la kuoka keki (cake pan) lenye ukubwa wa nchi 9, na upake siagi. Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka keki.

  Step4

  Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka keki ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 35 mpaka 40, au hadi utakapo ona keki imeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step5

  Keki ikisha iva, iondoe kwenye jiko la kuoka, kisha iweke pembeni ili ipoe, ikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka keki. Keki ikishapoa, unaweza kuitoa ndani ya sufuria la kuoka keki, na kuikata kwa ajili ya kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *