Jarida la Mapishi

Cupcakes za karanga na ndizi

 • Maandalizi
  Dakika 35
 • Kupika
  Dakika 25
 • Walaji
  12

Cupcakes za karanga na ndizi, ni cupcakes zenye ladha nzuri kama mkate wa ndizi, ambazo hupikwa kwa kutumia siagi ya karanga pamoja na ndizi. Cupckaes hizi zafaa kula kama kifungua kinywa wakati wa asubuhi, au kama kitafunio cha kawaida. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika, cupcakes hizi za karanga na ndizi.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, siagi ya karanga, ndizi, mafuta ya kupikia, mayai, pamoja na buttermilk, kisha changanya vizuri.

  Step2

  Weka vanilla extract, halafu endelea kuchanganya.

  Step3

  Weka unga wa ngano, light brown sugar, chumvi, pamoja na baking soda, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

  Step4

  Chukua sufuria la kuoka cupcakes (cupcakes pan) lenye matundu 12 ya cupcakes, na uweke ndani ya hayo matundu karatasi za kuokea cupcake (cupcake papers). Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka cupcakes.

  Step5

  Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka cupcakes ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 20 mpaka 25, au hadi utakapo ona cupcakes zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step6

  Cupcakes zikisha iva, ziondoe kwenye jiko la kuoka, kisha ziweke pembeni ili zipoe, zikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka cupcakes. Cupcakes zikishapoa, unaweza kuzitoa ndani ya sufuria la kuoka cupcakes, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *