Jarida la Mapishi

Muffins za machungwa na mpopi

Muffins za machungwa na mpopi | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Saa 1 Dk. 5
  • Kupika
    Dakika 25
  • Walaji
    12

Muffins za machungwa na mpopi, ni muffins tamu zilizo sheheni ladha ya machungwa. Muffins hizi ni rahisi sana kupika na zafaa sana kula kama kifungua kinywa wakati wa asubuhi, au kama kitafunio cha kawaida. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika muffins hizi za machungwa na mpopi.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria ndogo. Weka ndani ya hiyo sufuria maji pamoja na chungwa, halafu chemsha kwenye jiko lenye moto mkubwa, hadi utakapo ona chungwa limekuwa laini, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.

    Step2

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, chungwa ulilo lichemsha, mafuta ya nazi, mayai, pamoja na vanilla extract, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

    Step3

    Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli mchanganyiko ulio usaga.

    Step4

    Weka unga wa ngano, unga wa ngano ambao hauja kobolewa, chumvi, baking powder, pamoja na mbegu za mpopi, kisha changanya vizuri kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

    Step5

    Chukua sufuria la kuoka muffins (muffins pan), lenye matundu 12 ya muffins, na uweke ndani ya hayo matundu karatasi za kuokea muffin (muffin papers). Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka muffins.

    Step6

    Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka muffins ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 20 mpaka 25, au hadi utakapo ona muffins zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step7

    Muffins zikisha iva, ziondoe kwenye jiko la kuoka, kisha ziweke pembeni ili zipoe, zikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka muffins. Muffins zikishapoa, unaweza kuzitoa ndani ya sufuria la kuoka muffins, tayari kwa kula.

    Conclusion

    Hakikisha chungwa utakalo litumia unalichemsha pamoja na maganda yake. Usimenye kabisa maganda ya chungwa hilo.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.