Jarida la Mapishi

Keki ya chia na chocolate

 • Maandalizi
  Dakika 35
 • Kupika
  Dakika 40
 • Walaji
  10

Keki ya chia na chocolate, ni keki yenye ladha nzuri na rahisi sana kupika, inayopikwa kwa kutumia mbegu za chia pamoja na chocolate. Keki hii yafaa kula kama kitindamlo kwenye mlo wa jioni au katika sherehe. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza keki hii ya chia na chocolate.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, dark chocolate chips, pamoja na siagi, kisha weka bakuli hilo kwenye sufuria lenye maji ya moto, halafu acha siagi na chocolate viyeyuke. Ukiona siagi na chocolate vimeyeyuka, ondoa bakuli hilo kwenye sufuria lenye maji ya moto na uliweke pembeni.

  Step2

  Weka mayai, maganda ya chungwa, sukari na mafuta ya kupikia, kisha changanya vizuri.

  Step3

  Weka, cocoa powder, mbegu za chia, unga wa ngano, baking powder, pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

  Step4

  Chukua sufuria la kuoka keki (cake pan) lenye ukubwa wa nchi 9, na upake siagi. Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka keki.

  Step5

  Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka keki ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 35 mpaka 40, au hadi utakapo ona keki imeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step6

  Keki ikisha iva, iondoe kwenye jiko la kuoka, kisha iweke pembeni ili ipoe, ikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka keki. Keki ikishapoa, unaweza kuitoa ndani ya sufuria la kuoka keki, na kuikata kwa ajili ya kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *