Jarida la Mapishi

Keki ya limao

Keki ya limao | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 35
  • Kupika
    Dakika 40
  • Walaji
    10

Keki ya limao, ni keki nzuri inayofaa kuliwa kama kitinda mlo, wakati wowote au katika hafla yoyote ile. Keki hii hupikwa kwa kutumia sio tu limao iliyo kamuliwa, bali pia kwa kutumia maganda ya limao. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika keki hii ya limao.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, sukari pamoja na mayai, kisha changanya vizuri.

    Step2

    Weka siagi na uchanganye vizuri, kisha weka sour cream, vijiko 2 vya chakula vya maganda ya limao pamoja na vijiko 2 vya chakula vya limao iliyo kamuliwa, halafu endelea kuchanganya.

    Step3

    Weka unga wa ngano, baking powder pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri mchanganyiko huo kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

    Step4

    Chukua sufuria la kuoka keki (cake pan) lenye ukubwa wa nchi 9, na upake siagi. Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka keki.

    Step5

    Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka keki ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 35 mpaka 40, au hadi utakapo ona keki imeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step6

    Keki ikisha iva, iondoe kwenye jiko la kuoka, kisha iweke pembeni ili ipoe, ikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka keki. Keki ikishapoa, iondoe kwenye sufuria ya kuoka keki na uiweke kwenye sahani.

    Step7

    Chukua bakuli ndogo. Weka ndani ya hilo bakuli, powdered sugar, 1 kijiko cha chakula cha limao iliyo kamuliwa, pamoja na 1 kijiko cha chai cha maganda ya limao, kisha changanya vizuri, halafu mimina mchanganyiko huo juu ya keki. Baada ya hapo keki itakuwa tayari kwa ajili ya kukata na kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.