Jarida la Mapishi

Keki ya lozi

Keki ya lozi | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 35
  • Kupika
    Dakika 40
  • Walaji
    10

Keki ya lozi, ni keki laini iliyo sheheni ladha ya lozi. Keki hii hupikwa kwa kutumia lozi zilzo sagwa, asali, mdalasini, pamoja na lozi mbichi. Fuata hatua zifutazo ili ujifunze jinsi ya kupika keki hii ya lozi.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, siagi, asali, pamoja na sukari, kisha changanya vizuri.

    Step2

    Weka mayai, halafu endelea kuchanganya.

    Step3

    Weka unga wa ngano, lozi zilizo sagwa, baking powder, chumvi, mdalasini pamoja na lozi mbichi zilizo katwa katwa, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

    Step4

    Chukua sufuria la kuoka keki (cake pan) lenye ukubwa wa nchi 9, na upake siagi. Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka keki.

    Step5

    Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka keki ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 40, au hadi utakapo ona keki imeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step6

    Keki ikisha iva, iondoe kwenye jiko la kuoka, kisha iweke pembeni ili ipoe, ikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka keki. Keki ikishapoa, unaweza kuitoa ndani ya sufuria la kuoka keki, na kuikata kwa ajili ya kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.