Jarida la Mapishi

Ice cream ya nanasi

 • Maandalizi
  Dakika 15
 • Kupika
  -
 • Walaji
  2

Ice cream ya nanasi, ni ice cream inayo tengenezwa kwa kutumia matunda halisi ya nanasi, powdered sugar na krimu. Ice cream hii yafaa kuliwa kama kitindamlo katika msimu wa kiangazi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza ice cream hii ya nanasi.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, nanasi pamoja na powdered sugar, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vyema na kuwa laini.

  Step2

  Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena mchanganyiko wa nanasi ulio usaga pamoja na double cream, halafu changanya vizuri, kisha funika vizuri kontena hilo na uliweke kwenye friji kwa muda wa saa 4.

  Step3

  Baada ya saa 4, ondoa kontena hilo kwenye friji, kisha mimina mchanganyiko huo wa ice cream kwenye mashine ya kutengenezea ice cream (Ice Cream Maker Cooler). Washa mashine hiyo kwa muda wa dakika 40, au hadi utakapo ona ice cream imekuwa nzito na laini.

  Step4

  Ondoa ice cream hiyo kutoka kwenye mashine ya kutengeneza ice cream, kisha pakua kwenye bakuli safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *