Jarida la Mapishi

Keki ya cherry

 • Maandalizi
  Dakika 40
 • Kupika
  Dakika 20
 • Walaji
  8

Keki ya cherry, ni keki tamu yenye ladha nzuri ya cherry, inayopikwa kwa kutumia matumda halisi ya cherry. Keki hii yafaa kuliwa kama kitafunio cha kawaida, pamoja na juisi, smoothie, au milkshake. Ikiwa wewe ni mpenzi wa matunda ya cherry, basi nakuhakikishia utaipenda keki hii. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika keki hii ya cherry.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, siagi, pamoja na dark chocolate chips, kisha weka bakuli hilo kwenye sufuria lenye maji moto, hadi utakapo ona chocolate na siagi vimeyeyuka.

  Step2

  Weka mayai, vanilla extract, na light brown sugar, halafu endelea kuchanganya.

  Step3

  Weka unga wa ngano, chumvi, pamoja na matunda ya cherry, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

  Step4

  Chukua sufuria la kuoka keki (cake pan) lenye ukubwa wa nchi 8, na upake siagi. Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka keki.

  Step5

  Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka keki ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona keki imeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step6

  Keki ikisha iva, iondoe kwenye jiko la kuoka, kisha iweke pembeni ili ipoe, ikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka keki. Keki ikishapoa, unaweza kuitoa ndani ya sufuria la kuoka keki, na kuikata kwa ajili ya kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *