Jarida la Mapishi

Cupcakes za kahawa

Cupcakes za kahawa | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Saa 1 Dk. 10
  • Kupika
    Dakika 20
  • Walaji
    12

Cupcakes za kahawa, ni cupcakes rahisi sana kupika ambazo zimesheheni ladha ya kahawa. Cupcakes hizi zafaa kula kama kifungua kinywa wakati wa asubuhi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza cupcakes hizi za kahawa.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, mayai, pamoja na sukari, kisha changanya vizuri.

    Step2

    Weka vanilla extract, apple cider vinegar, maji, kahawa na mafuta ya kupikia, halafu endelea kuchanganya.

    Step3

    Weka unga wa ngano, cocoa powder, baking soda, pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

    Step4

    Chukua sufuria la kuoka cupcakes (cupcakes pan) lenye matundu 12 ya cupcakes, na uweke ndani ya hayo matundu karatasi za kuokea cupcake (cupcake papers). Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka cupcakes.

    Step5

    Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka cupcakes ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona cupcakes zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step6

    Cupcakes zikisha iva, ziondoe kwenye jiko la kuoka, kisha ziweke pembeni ili zipoe, zikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka cupcakes. Cupcakes zikishapoa, unaweza kuzitoa ndani ya sufuria la kuoka cupcakes, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.