Jarida la Mapishi

Ice cream ya machungwa

 • Maandalizi
  Dakika 30
 • Kupika
  -
 • Walaji
  4

Ice cream ya machungwa, ni ice cream tamu na laini, ambayo hutengenezwa kwa kutumia chungwa lililo kamuliwa na maganda yake kukunwa, kisha kusagwa. Ice cream hii yafaa sana kula kwenye sherehe ya birthday. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza ice cream hii ya machungwa.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua machungwa 4 na uyakate katikati kisha kamua juisi yake yote. Chukua chungwa moja lililobaki na ukune maganda yake (grate).

  Step2

  Chukua sufuria ndogo. Weka ndani ya hiyo sufuria, maganda ya machungwa uliyo yakuna, ⅔ kikombe cha maziwa, pamoja na sukari, kisha chemsha huku ukikoroga hadi utakapo ona sukari yote imeyeyuka. Epua mchanganyiko huo wa maziwa, kisha chukua chujio na uchuje mchanganyiko huo.

  Step3

  Chukua bakuli ndogo. Weka ndani ya hiyo bakuli viini vya mayai pamoja na double cream, kisha changanya vizuri mchanganyiko huo kwa kuupiga piga. Mimina mchanganyiko huu kwenye sufuria lenye mchanganyiko wa maziwa.

  Step4

  Weka maziwa yaliyobaki ambayo huku yachemsha, halafu changanya tena vizuri kwa kuupiga piga mchanganyiko huo, kisha acha upoe.

  Step5

  Ukiona mchanganyiko huo umepoa, weka juisi ya machungwa uliyo ikamua, kisha changanya tena kwa kuupiga piga mchanganyiko huo, hadi utakapo ona umechanganyika vizuri na kuwa laini.

  Step6

  Mimina mchanganyiko huo wa ice cream kwenye mashine ya kutengenezea ice cream (Ice Cream Maker Cooler). Washa mashine hiyo kwa muda wa dakika 40, au hadi utakapo ona ice cream imekuwa nzito na laini.

  Step7

  Ondoa ice cream hiyo kutoka kwenye mashine ya kutengeneza ice cream, kisha pakua kwenye bakuli safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *