Jarida la Mapishi

Ice cream ya blueberry

 • Maandalizi
  Dakika 10
 • Kupika
  -
 • Walaji
  4

Ice cream ya blueberry, ni ice cream inayo tengenezwa kwa kutumia matunda halisi ya blueberry yaliyo sagwa pamoja na krimu. Ice cream hii yafaa kula kama kitindamlo kipindi cha kiangazi au katika msimu wa matunda ya blueberry. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza ice cream hii ya blueberry.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, limao, matunda ya blueberry, sukari, maziwa, pamoja na double cream, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vyema na kuwa laini.

  Step2

  Mimina mchanganyiko huo wa ice cream kwenye mashine ya kutengenezea ice cream (Ice Cream Maker Cooler). Washa mashine hiyo kwa muda wa dakika 50 mpaka 60, au hadi utakapo ona ice cream imekuwa nzito na laini.

  Step3

  Ondoa ice cream hiyo kutoka kwenye mashine ya kutengeneza ice cream, kisha pakua kwenye bakuli safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *