Jarida la Mapishi

Keki ya apple

 • Maandalizi
  Dakika 35
 • Kupika
  Dakika 40
 • Walaji
  10

Keki ya apple, ni keki tamu na laini ambayo imepikwa kwa kutumia matunda halisi ya apple pamoja unga wa ngano na mdalasini ambavyo hufanya keki hii iwe na ladha ya kipekee zaidi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika keki hii ya apple.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua bakuli la kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, unga wa ngano, baking powder, mdalasini, tangawizi, pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri.

  Step2

  Chukua bakuli nyingine ndogo. Weka ndani ya hiyo bakuli siagi, sukari, maple syrup na uchanganye vizuri, kisha weka maziwa pamoja na mayai, na uchanganye tena vizuri.

  Step3

  Chukua mchanganyiko wa bakuli ndogo ya pili, na umimine kwenye mchanganyiko wa bakuli la kwanza. Weka apple pamoja na jozi (walnuts) kwenye hilo bakuli la kwanza, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

  Step4

  Chukua sufuria la kuoka keki (cake pan) lenye ukubwa wa nchi 9, na upake siagi. Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka keki.

  Step5

  Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka keki ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 35 mpaka 40, au hadi utakapo ona keki imeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step6

  Keki ikisha iva, iondoe kwenye jiko la kuoka, kisha iweke pembeni ili ipoe, ikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka keki. Keki ikishapoa, unaweza kuitoa ndani ya sufuria la kuoka keki, na kuikata kwa ajili ya kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *