Jarida la Mapishi

Ice cream ya strawberry na mrehani

 • Maandalizi
  Dakika 10
 • Kupika
  -
 • Walaji
  4

Ice cream ya strawberry na mrehani, ni ice cream tamu yenye krimu ambayo hutengenezwa kwa kutumia matunda halisi ya strawberry pamoja na mmea wa mrehani. Ice cream hii yafaa kula kama kitindamlo baada ya mlo wowote ule kwenye msimu wa kiangazi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza ice cream hii ya strawberry na mrehani.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, ndizi, matunda ya strawberry, double cream, pamoja na majani ya mrehani, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

  Step2

  Chukua kontena kubwa. Weka mchanganyiko ulio usaga ndani ya hilo kontena. Weka na apple syrup kadiri ya mahitaji yako, kisha changanya vizuri.

  Step3

  Funika kontena vizuri, kisha weka mchanganyiko huo wa ice cream kwenye freezer kwa muda wa dakika 5 mpaka 10.

  Step4

  Baada ya dakika 5 au 10, ondoa kontena hilo kwenye freezer, kisha mimina mchanganyiko huo wa ice cream kwenye mashine ya kutengenezea ice cream (Ice Cream Maker Cooler). Washa mashine hiyo kwa muda wa dakika 40 mpaka 50, au hadi utakapo ona ice cream imekuwa nzito na laini.

  Step5

  Ondoa ice cream hiyo kutoka kwenye mashine ya kutengeneza ice cream, kisha pakua kwenye bakuli safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *