Jarida la Mapishi

Viazi vyenye kitunguu na nyanya

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 45
 • Walaji
  4

Viazi vyenye kitunguu na nyanya, ni chakula kizuri kilicho sheheni wanga, ambacho hupikwa kwa kutumia viazi mviringo vilivyo chemshwa, kitunguu, nyanya, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika viazi hivi vyenye kitunguu na nyanya.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria viazi mviringo pamoja na maji, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona vimeiva.

  Step2

  Epua na umwage maji yote yaliyomo kwenye sufuria na kubakiwa na viazi peke yake, kisha acha vipoe.

  Step3

  Menya maganda ya viazi hivyo, kisha vikate katika vipande vidogo vidogo.

  Step4

  Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka vitunguu maji kwenye hicho kikaango, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona vimeiva.

  Step5

  Weka nyanya, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 4, au hadi utakapo ona mchuzi umekuwa mzito.

  Step6

  Weka binzari ya manjano, binzari nyembamba, mbegu za giligilani, pamoja na chumvi, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

  Step7

  Weka viazi mviringo ulivyo vichemsha pamoja na majani ya giligilani, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona viazi mviringo vimechanganyika vyema pamoja na vitunguu maji na nyanya.

  Step8

  Nyunyizia garam masala halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *