Jarida la Mapishi

Viazi mviringo vya kukaanga

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 50
 • Walaji
  4

Viazi mviringo vya kukaanga, ni chakula kizuri ambacho hupikwa kwa kuchanganywa na viungo, ambavyo huvifanya viazi hivi viwe na ladha nzuri zaidi. Fauata hatua zifuatazo, ili kujifunza jinsi ya kupika hivi viazi mviringo vya kukaanga.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria viazi mviringo pamoja na maji, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona vimeiva.

  Step2

  Epua na umwage maji yote yaliyomo kwenye sufuria na kubakiwa na viazi peke yake, kisha acha vipoe. Viazi vikishapoa, menya maganda yake yote, kisha vikate katika vipande vidogo vidogo.

  Step3

  Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka vitunguu maji kwenye hicho kikaango, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona vitunguu vimeiva.

  Step4

  Weka nyanya, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 4.

  Step5

  Weka garam masala, binzari ya manjano, binzari nyembamba, mbegu za giligilani, pamoja na chumvi, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

  Step6

  Weka viazi mviringo pamoja na majani ya giligilani, kisha endelea kupika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona viazi vimechanganyika vyema pamoja na vitunguu maji na nyanya.

  Step7

  Epua mchanganyiko huo wa viazi na uweke kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *