Jarida la Mapishi

Saladi ya njegere na viazi

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 50
 • Walaji
  4

Saladi ya njegere na viazi, ni aina ya saladi ambayo asili yake ni kutoka nchini India. Saladi hii hutengezwa kwa kutumia njegere, viazi mviringo vitamu, viazi vitamu, pamoja na viungo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza saladi hii ya njegere na viazi.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria la ukubwa wa wastani. Weka kwenye hilo sufuria maji ya kutosha, chumvi kiasi, pamoja na viazi mviringo, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 15, au hadi utakapo ona viazi vimeiva. Epua viazi hivyo na umwage maji yote yaliyomo kwenye sufuria, kisha acha vipoe. Viazi vikishapoa, vimenye maganda yake yote na kuvikata katika vipande vidogo vidogo.

  Step2

  Chukua sufuria jingine la ukubwa wa wastani. Weka kwenye hilo sufuria maji ya kutosha, chumvi kiasi, pamoja na viazi vitamu, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 15 mpaka 20, au hadi utakapo ona viazi vimeiva. Epua viazi hivyo na umwage maji yote yaliyomo kwenye sufuria, kisha acha vipoe. Viazi vikishapoa, vimenye maganda yake yote na kuvikata katika vipande vidogo vidogo.

  Step3

  Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hicho kikaango viazi mviringo pamoja na viazi vitamu, kisha kaanga viazi hivyo huku ukivigeuza geuza geuza mara kwa mara kwa muda wa dakika 7, au hadi utakapo ona vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Epua viazi hivyo na uviweke kwenye sahani ili vipoe.

  Step4

  Weka njegere kwenye hicho hicho kikaango, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 4, au hadi utakapo ona njegere zimeanza kubadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step5

  Weka viazi mviringo pamoja na viazi vitamu ulivyo vikaanga mwanzoni kwenye hicho kikaango chenye njegere. Weka pia Tamarind Paste, chumvi, Chaat Masala, pamoja na majani ya giligilani, kisha kaanga huku ukigeuza mara kwa mara kwa muda wa dakika 2.

  Step6

  Epua mchanganyiko huo na uweke kwenye kontena. Weka kwenye hilo kontena vitunguu maji na uchanganye vizuri, kisha acha ipoe kabla ya kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *