-
Maandalizi-
-
KupikaSaa 1 Dk. 10
-
Walaji4
Mchuzi wa nyama ya nguruwe, ni pishi tamu na rahisi kupika, ambalo hupikwa kwa kutumia nyama ya nguruwe, ukwaju, nazi, vitunguu maji, pamoja viungo. Mchuzi huu wafaa kula pamoja na wali, ugali, au chakula kingine chochote upendacho. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mchuzi huu wa nyama ya nguruwe.
Ingredients
Directions
Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka kwenye hicho kikaango, mbegu za giligilani, mbegu za binzari nyembamba, mbegu za haradali, pamoja na mbegu za pilipili manga, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 2, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka mchanganyiko ulio ukaanga kwenye hiyo mashine ya kusaga, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri.
Weka binzari ya manjano, mdalasini, kungumanga, pamoja na chumvi, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umechanganyika vyema. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na uweke pembeni kwenye kontena.
Weka kwenye hiyo hiyo mashine ya kusaga, ½ ya vitunguu maji, tangawizi, vitunguu swaumu, tui la nazi, pamoja na Tamarind Paste, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.
Weka mchanganyiko wa viungo uliomo kwenye kontena, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umechanganyika vyema.
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka ½ ya vitunguu maji vilivyobaki kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Weka mchanganyiko ulio usaga, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Weka nyama ya nguruwe, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 15, au hadi utakapo ona nyama imebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Mimina maji halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, halafu funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 30, au hadi utakapo ona nyama imeiva na mchuzi umekuwa mzito, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review