-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 35
-
Walaji4
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mdalasini, iliki, tangawizi, vitunguu swaumu, korosho, pamoja na pistachio, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5.
Mimina mtindi taratibu huku ukikoroga, kisha acha ichemke huku ukikoroga mara kwa mara, hadi utakapo ona mtindi umekaribia kukauka.
Weka zabibu kavu, garam masala, kungumanga, nyama ya kusaga, chumvi, pamoja na pilipili manga, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5.
Weka tomato sauce halafu koroga vizuri, kisha acha ichemke kwa muda wa dakika 2 mpaka 3.
Punguza moto na uweke moto mdogo, kisha acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona nyama imeiva. Epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Conclusion
Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.
Leave a Review