-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 55
-
Walaji4
Mchuzi wa mbavu, ni kitoweo kitamu na rahisi kupika, ambacho hupikwa kwa kutumia mbavu za mbuzi, au mbavu za kondoo, au mbavu za nguruwe. Kitoweo hiki chafaa kula pamoja na wali mweupe, mkate au tambi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mchuzi huu wa mbavu.
Ingredients
Directions
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, lozi, binzari nyembamba, mbegu za giligilani, pamoja na mbegu za mpopi, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri.
Weka tangawizi, vitunguu swaumu, pamoja na ¼ kikombe cha maji, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.
Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria nyama za mbavu, vitunguu maji, pilipili manga, mdalasini, karafuu, chumvi, pamoja na maji halafu koroga vizuri, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 40, au hadi utakapo ona nyama imeiva. Ondoa nyama za mbavu kwenye sufuria na uziweke pembeni kwenye kontena, kisha epua sufuria lenye supu na uliweke pembeni.
Chukua sufuria jingine kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka mchanganyiko wa lozi ulio usaga kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona imebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Mimina tui la nazi pamoja na supu, halafu koroga vizuri, kisha acha ichemke kwa muda wa dakika 5.
Weka nyama za mbavu pamoja na Tamarind Paste halafu koroga vizuri, kisha acha ichemke kwa muda wa dakika 5.
Nyunyizia garam masala halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review