-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 35
-
Walaji4
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka vitunguu maji kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Weka majani ya mvuje, tangawizi, vitunguu swaumu, pamoja na nazi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.
Weka vipande vya nyama ya kuku, binzari ya manjano, pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukivigeuza vipande vya nyama ya kuku mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Mimina tui la nazi halafu koroga vizuri, kisha funika sufuria na uache ichemke kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona vipande vya nyama ya kuku vimeiva. Epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review