-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 45
-
Walaji4
Ingredients
Directions
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, vitunguu maji, unga wa dengu, mdalasini, pamoja na karafuu, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na uweke pembeni kwenye kontena.
Weka kwenye hiyo hiyo mashine ya kusaga, tangawizi, vitunguu swaumu, lozi, 1 kijiko cha chakula cha mafuta ya kupikia, pamoja na chumvi, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.
Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena, vipande vya nyama ya kuku pamoja na mchanganyiko wa tangawizi ulio usaga, kisha changanya vizuri hadi utakapo ona vipande vyote vya nyama ya kuku vimeenea vyema viungo. Funika vizuri kontena hilo, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 4 mpaka saa 24.
Chukua sufuria kubwa lenye vijiko 2 vya chakula vya mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka vipande vya nyama ya kuku kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Weka mchanganyiko wa vitunguu maji ulio usaga, kisha mimina mtindi taratibu huku ukikoroga.
Punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache ichemke kwa muda wa dakika 15, au hadi utakapo ona mtindi umekauka. Kumbuka kukoroga mara 1 au 2 wakati inachemka.
Mimina tui la nazi halafu koroga vizuri, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 20 zaidi au hadi utakapo ona vipande vya nyama ya kuku vimeiva, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Conclusion
Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.
Leave a Review