Jarida la Mapishi

Mchuzi wa kondoo

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Saa 1 Dk. 25
 • Walaji
  4

Mchuzi wa kondoo, ni pishi ambalo hupikwa kwa kutumia nyama ya kondoo, nyanya, vitunguu maji, nazi, pamoja na viungo. Ingawa pishi hili huchukua mda kupika, nakuhakikishia mara baada ya kumaliza kupika pishi hili, utafurahia mchuzi mtamu wa kondoo wenye ladha na harufu nzuri ya kupendeza. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika mchuzi huu wa kondoo.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, vitunguu maji, tangawizi, vitunguu swaumu, majani ya giligilani, pamoja na majani ya mvuje, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

  Step2

  Weka nyanya, garam masala, binzari ya manjano, pamoja na chumvi, kisha endelea kusaga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umesagika vyema na kuwa laini.

  Step3

  Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria iliki pamoja na pilipili manga, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

  Step4

  Weka binzari nyembamba, mbegu za haradali, pamoja na nyama ya kondoo, kisha kaanga huku ukigeuza geuza nyama mara kwa mara kwa muda wa dakika 15, au hadi utakapo ona nyama imebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

  Step5

  Weka mchanganyiko ulio usaga, kisha pika mchanganyiko huo wa nyama ya kondoo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika dakika 18 mpaka 20.

  Step6

  Weka maji na ukoroge vizuri, kisha funika sufuria na acha ichemke kwa muda wa dakika 30 mpaka 40, au hadi utakapo ona nyama ya kondoo imeiva na mchuzi umekuwa mzito.

  Step7

  Weka tui la nazi na ukoroge vizuri, halafu acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 5 zaidi, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *