Jarida la Mapishi

Juisi ya limao ya rosemary

 • Maandalizi
  Dakika 10
 • Kupika
  -
 • Walaji
  1

Juisi ya limao ya rosemary, ni juisi ambayo itashangaza watu wengi wanao ufahamu mmea wa rosemary. Najua hapo ulipo unawaza kichwani mwako, rosemary kwenye juisi? Ndio. Majani ya rosemary, husaidia kuyafanya malimao yawe na ladha nzuri zaidi. Ikiwa wewe ni mpenzi wa mmea wa rosemary, basi nakuhakikishia utaipenda juisi hii. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza juisi hii ya limao ya rosemary.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, limao, matunda ya apple, majani ya rosemary, maji, pamoja na sukari, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wa juisi umesagika vizuri.

  Step2

  Chuja juisi kwa kutumia chujio, kisha iweke kwenye friji ili ipate baridi kabla ya kunywa.

  Conclusion

  Unaweza kuongeza maji kwenye juisi hii kadiri upendavyo, endapo utaona maji yaliyomo katika juisi hii ni kidogo.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *