Jarida la Mapishi

Juisi ya limao ya karoti

 • Maandalizi
  Dakika 10
 • Kupika
  -
 • Walaji
  1

Juisi ya limao ya karoti, ni juisi nzuri yenye afya, inayo tengenewa kwa kutumia karoti, limao na apple. Juisi hii yafaa kunywa kama kifungua kinywa wakati wa asubuhi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza juisi hii ya limao ya karoti.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, karoti, limao, apple, maji, pamoja na sukari, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wa juisi umesagika vizuri.

  Step2

  Chuja juisi kwa kutumia chujio, kisha iweke kwenye friji ili ipate baridi kabla ya kunywa.

  Conclusion

  Unaweza kuongeza maji kwenye juisi hii kadiri upendavyo, endapo utaona maji yaliyomo katika juisi hii ni kidogo.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Recipe Reviews

  • Noela

   Asante sana Kwa MAARIFA,Nina swali,lmao umeliosha na kuliweka na maganda yake au umekamua juisi yake ukaiweka kwenye apple na karoti ndani ya Brenda? Asante

   • Mary Joachim

    Unaweza ukamenya limao maganda yake yote kama chenza kisha ukalikata kata na kuliweka kwenye blender, au unaweza kulikamua limao na juisi yake ukaiweka kwenye blender.

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *