Jarida la Mapishi

Chai ya viungo

 • Maandalizi
  -
 • Kupika
  Dakika 10
 • Walaji
  2

Chai ya viungo, ni chai ya asili ya India ambayo hupikwa kwa kuchanganya viungo, maziwa pamoja na sukari. Ikiwa wewe ni mpenzi wa chai, usiache kunywa chai hii wakati wa asubuhi, ili uweze kupata nguvu na ari ya kufanya shughuli zako za siku nzima. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza chai hii ya viungo.

Ingredients

  Directions

  Step1

  Chukua sufuria la ukubwa wa wastani. Weka ndani ya hilo sufuria, maziwa, mbegu za shamari, tangawizi, mdalasini, maji, iliki, pamoja na pilipili manga, kisha weka hilo sufuria kwenye jiko lenye moto mkubwa na uache ichemke. Ukiona inaanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, halafu acha iendelee kuchemka kwa dakika 1 zaidi, kisha epua na uweke pembeni.

  Step2

  Weka majani ya chai ndani ya hilo sufuria, kisha funika sufuria na uache kwa muda wa dakika 3 ili majani ya chai yapate kuchanganyika vizuri pamoja na maji ya moto yenye viungo. Baada ya dakika 3, funua mfuniko na ukoroge vizuri, kisha chuja chai kwenye vikombe tayari kwa kunywa.

  Conclusion

  Unaweza kutumia asali au sukari katika chai hii, kadiri utakavyo ona inafaa.

  Unaweza Pia Kusoma Hizi

  Leave a Review

  Your email address will not be published. Required fields are marked *